ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

Kuhusu CRDB Bank Marathon

CRDB Bank Marathon ni mbio za kimataifa zinazotoa fursa kwa jamii, wateja, taasisi washirika watanzaniana washirika duniani kote kushirikiana na Benki ya CRDB kutoa mchango katika jamii katika nyanja za elimu, afya na mazingira.CRDB Bank Marathon ni fursa kwa jamii na dunia nzima kusaidia kuboresha jamii yetu na kusambaza tabasamu kwa watu wenye uhitaji. Karibu tusambaze tabasamu! 

Ujumbe kutoka Menejimenti

Kupitia sera yetu ya kusaidia jamii, tumekuwa tukishiriki katika kuboresha maisha ya jamii yetu na kuleta maendeleo katika nyanja za elimu, afya, na mazingira. Marathon ya Benki ya CRDB inatupa fursa ya kushirikiana na wateja wetu, wadau wa biashara na Watanzania wote katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu zaidi.

Mbio za mwaka huu za CRDB Bank Marathon zinatarajiwa kukusanya takriban bilioni moja za Kitanzania ambazo zitakwenda kusaidia Sekta ya Afya kwa upande wa Mama na Mtoto visiwani Zanzibar. Pia, kampeni ya CCBRT ya kuboresha matokeo ya afya ya uzazi kwa wanawake wenye ujauzito hatarishi (High Risk Pregnancy). Vilevile, uchangiaji wa gharama za upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Abdulmajid Mussa Nsekela

Tully Esther Mwambapa

Mkurugenzi wa Mawasiliano.

Mkurugenzi Mtendaji.