ENG

ENG

ENG

 • Mwanzo
 • Kuhusu
 • Mbio
 • Habari na Picha
 • Matokeo
 • Wadhamini
 • Wasiliana Nasi

ENG

ENG

ENG

Azimio la Fidia

Ninathibitisha kukubaliana na taarifa zilizoorodheshwa hapa chini kuwa;

 • Nimesoma kanuni na masharti ya kushiriki katika CRDB Bank Marathon na ninakubali kushiriki kwa uelewa kwamba nitangatia masharti yote yaliyoorodheshwa.
 • Ninaelewa kuwa kwa kukubali kanuni na masharti haya, ninakubali utumiaji wa taarifa zangu binafsi, picha, au rekodi zingine za tukio hili kwa madhumuni yoyote halali, ikiwamo matangazo ya kibiashara, uuzajiwa bidhaa zinazotolewa na mratibu wa CRDB Bank Marathon na wadhamini
 • Ninaelewa changamoto zinazoambatana na kukimbia/ kuendesha baiskeli hivyo nitashiriki kwa hiari yangu na kuwa nitawajibika binafsi kwa yatakayotokea.
 • Mimi ni mzima wa mwili na nina uwezo wa kushiriki katika mbio hizi na sijashauriwa vinginevyo na daktari aliye na sifa.

 

 • Sitawasilisha malalamiko yoyote kuhusiana na changamoto zitakazojitokeza katika mbio hizi, wala kuwasilisha mashtaka katika vyombo vya kisheria, binafsi au kupitia wanasheria  wangu.
 • Ikiwa nimeumia au kuugua, naidhinisha waandaji wa mbio hizi na maafisa kunisafirisha kwenda katika kituo cha matibabu au hospitalini na kuondoa madai yote ambayo yanaweza kusababishwa na usafiri, ucheleweshaji au mapungufu yatokanayo na matibabu.
 • Ikiwa nina mtoto/ kijana chini ya miaka 18 kwenye uangalizi wangu, basi nitahakikisha kuwa wanaongozana wakati wote na mtu mzima anayewajibika na kuelewa kanuni na taratibu za mbio hizi.
 • Natamka kwamba taarifa zote nilizowasilisha ni sahihi na ninathibitisha kwamba ninakubaliana na kanuni na masharti yote ya mbio hizi.

 

Haki zote zimehifadhiwa.