ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

Sera ya Faragha

1. Muhtasari

Tafadhali soma Sera hii ya Faragha ili kuelewa namna ambavyo taarifa zinazokusanywa kupitia tovuti hii ya CRDB Bank Marathon zinatumika.

2. Ukusanyaji wa taarifa binafsi

Katika tovuti hii ya CRDB Bank Marathon tunakusanya aina zaidi ya moja ya taarifa binafsi kama ifuatavyo;

  • Jina, anwani ya barua pepe, namba ya simu au utambulisho mwingine.
  • Utambulisho binafsi wa mtandao, taarifa za anwani ya mtandao, historia na taarifa kutembelea tovuti.

 

3. Kuwasiliana nasi

Taarifa binafsi kama jina, barua pepe, anwani ya makazi na namba ya simu zitahifadhiwa pindi unapowasiliana nasi kwa ajili ya;

  • Kutoa mrejesho wa maswali au changamoto
  • Kuboresha tovuti yetu au huduma nyingine
  • Kufuatilia maswali tunayopokea na mawasiliano zaidi

 

Ikiwa utahitaji kuwasiliana nasi unashauriwa kutumia barua pepe [email protected] au namba ya simu +255714197700/ +255755197700.

4. Ukusanyaji wa Habari ya kibinafsi kutoka kwa Watoto

Kwa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 18 anapaswa kupata idhini kutoka kwa mzazi au mlezi kuhusu kutoa taarifa zake katika tovuti au mzazi au mlezi kutoa taarifa kwa niaba.

5. Haki ya kuwasiliana na mtumiaji

Tuna haki ya kuwasiliana na watu wote wanaotembelea tovuti yetu kuhusu mabadiliko ya sera hii ya faragha ili kuhakikisha wanaielewa na kuridhia.

6. Usalama

Tunahakikisha tunalinda taarifa binafsi za watembeleaji wa tovuti yetu; kuzuia mtu/ watu wasioruhusiwa kufika taarifa kutumika vibaya.

7. Wasiliana Nasi

Ikiwa una swali lolote kuhusu Sera hii ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe [email protected]