ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

ENG

CRDB Bank Marathon 2021 yafanikiwa kukusanya nusu bilioni kusaidia afya na mazingira

Dar es Salaam 15 Agosti 2021 - Mbio za hisani za kimataifa zilizoandaliwa na Benki ya CRDB “CRDB Bank International Marathon” kwa mwaka 2021 zimefanikiwa kuandika rekodi kwa kuvutia washiriki zaidi ya 5,000 ikiwamo maelfu ya raia wa kigeni. Jumla ya Shilingi za Kitazania Shilingi milioni 500 zimefanikiwa kukusanywa ambazo zitaelekezwa kwa ajili ya kusaidia jamii.Akizungumza na washiriki, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mbio hizo, aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Benki ya CRDB kwa kufanikisha mbio hizo zilizokuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo JKCI, kujenga kituo cha mawasiliano cha Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na kusaidia utunzaji mazingira kupitia kampeni ya Pendezesha Tanzania. Waziri Majaliwa alisema kuwa Serikali inasikia fahari kuona taasisi za kizalendo kama Benki ya CRDB zikiwa mstari wa mbele katika kusaidia Serikali kuboresha sekta za kijamii kama vile; afya, elimu na mazingira na huku akikiri kwa dhati kuwa mbizo hizo zinazofanyika kila mwaka kuwa ni fursa adhimu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwekeza katika ustawi wa jamii.“Nimekuja hapa kwa lengo la kuonyesha kuwa Serikali inaunga mkono na kufurahishwa sana na ubunifu huu wa Benki ya CRDB. Kwa niaba ya Serikali niwashukuru kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) kwa kuboresha huduma za afya kwa umma,” anaeleza Waziri Mkuu.

Aliwapa kongole viongozi mbalimbali wa Serikali ikiwamo; Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Naibu Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Pauline Gekul, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel na washiriki wengine wote kwa kuunga mkono jitihada hizo ambazo zimejielekeza katika kuokoa maisha ya wale wenye uhitaji katika jamii na kuboresha mazingira.“Nafahamu wazi kuwa ni ngumu miongoni mwenu kuamka asubuhi sana hususan katika hali hii ya hewa ya baridi na siku za mapumziko, lakini mmeweza kuzishinda nafsi zenu na kuacha shuka zenu pembeni ili kuja kushiriki katika mbio hizi,” aliongezea.Alipongeza uamuzi wa Benki ya CRDB kuendelea kusaidia upasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo. Waziri Mkuu alisema uamuzi huo utaendelea kusaidia kupunguza makali ya gharama kwa ajili ya upasuaji wa moyo ambazo watu wengi hawawezi kuzimudu  pamoja na Serikali kutoa ruzuku ya asilimia 80.“Wazo hili la kuendelea kusaidia gharama za upasuaji kwa watoto ni uamuzi mzuri sana kwani hata asilimia 20 iliyobaki wazazi wengi hawana uwezo wa kuchangia. Hongereni kwa kurejesha tabasamu kwa watoto na kuwapatia tumaini la maisha,” Waziri Majaliwa alisisitiza. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alibainisha kuwa mbizo za mwaka huu zimevuka lengo la ukusanyaji wa Shilingi milioni 500, akitoa shukrani kwa makampuni na taasisi zilizojitokeza kushirikiana na benki hiyo pamoja na wakimbiaji waliojitokeza kutoka ndani na nje ya nchi muda wa 01:03:19, kwa upande wa wanawake mshindi alikuwa Pauline Esikon raia wa Kenya baada ya kutumia muda wa 01:12:17.Katika10km, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Joseph Tiophil raia wa Tanzania alitumia muda wa 00:28:51, kwa wanawake Transfora Musa raia wa Tanzania ameshika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa 00:33:52. Katika mashindano ya mbio za baiskeli 65km, Masunga Duba raia wa Tanzania aliibuka mshindi kwa upande wa wanaume baada ya kutumia muda wa 01:49:07, upande wa wanawake Swabra Abdallah raia wa Tanzania ameibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 02:06:39. Washindi 32 katika mbio hizo wamejizolea jumla ya Shilingi Milioni 50.